Wananchi Wilaya ya Kusini wametakiwa kuwaenzi Viongozi walioitumiakia Nchini na kuleta maendeleo katika Serikali.
Hayo yameelezwa na Mhe.Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Mhe.Nadir Abdul-latif katika Dua maalum ya kumuombea Raisi wa Awamu ya Nne Sheikh Idrissa Abduli Wakili katika Kaburi lake liopo Kiongoni.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inawajibu wa kuwaombea Dua Viongozi hao kila ifikapo Mwezi wa Nne wa kila Mwaka ambapo ni utaratibu wao waliojiwekea kama ni sehemu ya kuwaenzi.
Akizungumza kwa niaba ya Familia Mtoto wa Marehemu Ndg.Yahya Idrissa Abduli-wakili ameishukuru Serikeli kwa kuona umuhimu wa kuwaenzi Viongozi hao jambo ambalo linaleta faraja.
stories
standard