Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mh. Tabia Maulid Mwita, amefanya ziara ya kustukia katika Ofisi za Baraza la Michezo na Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni na kupokea changamoto mbalimbali zinazowakabili Wafanyakazi wa Taasisi hizo.
Hayo yamejiri huko Baraza la Michezo Mwanakwerekwe, Ambapo Waziri Tabia baada ya kupokea malalamiko hayo amewataka Viongozi wa Taasisi hizo kuyatatua mara moja huku akisisitiza uwajibikaji katika kwa lengo la kupatikana ufanisi.
Mara baada ya Ziara hiyo Mh. Waziri amekutana na Uongozi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, na kufanya mazungumzo nao juu ya Mikakati mbalimbali ikiwemo suala la Kanuni ya ZBC na ya Waziri na masuala ya Posho za Wafanyakazi.
stories
standard