MAFANIKIO SHIRIKA LA RELI TANZANIA MIAKA MITATU YA RAIS SAMIA

MKURUGENZI SHIRIKA LA RELI TANZANIA

Shirika la Reli Tanzania  TRC limesema katika kipindi cha Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Shirika hilo limefanikisha kujenga Kilomita 1,560 za Mradi wa Reli ya kisasa  ya SGR.

Mafanikio hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika  hilo  Masanja Kadogosa  amesema Thamani ya uwekezaji wa Mradi huo imefikia Trioni 23.3ukiondoa kipande cha Uvinza hadi Musongati ambapo kipo katika  hatua ya ununuzi ambapo kati ya fedha hizo jumla ya Shilingi Trioni 10.01 zimeshalipwa kwa Wakandarasi .

Amesema kiujumla utekelezaji wa ujenzi unaoendelea kwa  vipande vitano vipya ambapo vitatu  ni katika kukamilisha  ujenzi wa awamu  ya kwanza ya Reli SGR kati ya  Dar Es Salam hadi Mwanza ambapo ,Makutupora hadi Tabora( km368) Ujenzi  umefikia asilimia 13.98,Tabora hadi Isaka( km 165)  umefikia asilimia 5.44na Isaka hadi Mwanza( km341) ambapo Ujenzi umefikia asilimia 54.01  .   

Akizungumzia  Ukarabati wa  Reli ya zamani( MGR) Mkurugenzi Kadogosa amesema Serikali ya awamu ya Sita  imetowa fedha kwa ajili ya ukarabati wa Mabehewa zaidi ya Mia Sita kati ya hayo Mabehewa Mia Mbili Tayari yameshafanyiwa ukarabati  .

Shirika la Reli Tanzania linaendelea kuhakikisha usafiri wa Abiria na Mizigo unaendelea kwa ufanisi ili kutimiza malengo na maadhimio ya Shirika  hilo kwa  kutoa huduma bora na  yakuaminika ya usafiri wa Reli Nchini.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.