WEMA IMEWATAKA WAHITIMU KIDATO CHA SITA KUTUMIA FURSA WALIZOZIPATA

WAZIRI LELA MOHAMED MUSSA

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imewataka Wahitimu  Waliofaulu Kidatu cha Sita  kutumia vyema fursa walizozipata za kuendelea na Masomo ya Elimu ya juu  ili kutimiza malengo  yao na ya  Serikali ya kuzalisha Wataalamu mahiri.

Akizungumza katika Sherehe ya kuwapongeza Wanafunzi waliohitimu Kidatu cha Sita Skuli ya Lumumba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh Lela Mohammed Mussa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  inafanya juhudi kubwa za kuhakikisha sekta ya Elimu inaendelea hivyo ni vyema kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao waliokusudia.

Muakilishi wa Jimbo la Malindi Mohammed Ahmada Salum amewapongeza Walimu kwa kazi wanayoifanya  ya kuwapata Wanafunzi Elimu bora 

Amesema hatua hiyo itawezesha kupatikana Wataalamu wenye sifa na kukuza uchumi wa Nchi 

Nao Mkuu wa Skuli hiyo  Mussa Hassan Musa na Mwanafunzi wa Skuli hiyo Tunu Kasimu Paulo ni Mwanafunzi Skuli ya Lumumba na Mwalimu  wamesema kwa asilimia kubwa ufaulu  wa Wanafunzi umeongezeka jambo ambalo linawapa matumaini makubwa ya  kuongeza za juhudi ya kusoma kwa bidiii 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.