Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuhifadhi Qur-an Tukufu na kufundisha Wwatoto wao pamoja na kutoa Sadaka kwa Watu wenye mahitaji.
Dkt.Mwinyi amesema hayo katika Fainali ya 24 ya Mashindano ya Qur-an Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Al-hikma Foundation kwa kushirikisha Nchi za Afrika na Nje ya Afrika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar-es- salaam pamoja na kuwaomba Watanzania kuendeleza mshikamano, umoja na kutunza amani iliyopo.
Aidha Rais wa Zanzibar ameipongeza Benki ya Watu wa Zanzibar (Pbz) kwa kuyadhamini Mashindano hayo kila Mwaka.
Mshindi wa Kwanza wa Mashindano hayo ni Ndg.Ibrahim Sow wa Ivory Coast aliyepata Shilingi Milioni 27, Mshindi wa Pili ni Ndg.Haafith Abdulkariim Kabiito kutoka Uganda na Mshindi wa Tatu ni Ndg.Kamil Almin Swaleh kutoka Tanzania