Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla amewaasa Wanafunzi wa Kidato cha Sita kuzidisha juhudi katika Masomo yao ili kupata Viongozi bora wa baadae.
Ameyasema hayo wakati akikabidhi Futari kwa Wanafunzi wanaoishi Dahalia mbali mbali Kisiwani Pemba kwa lengo la kuwarahisishia upatikanaji wa Ftari katika kipindi hichi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Amesema Serikali imeamua kuftari na Wanafunzi wanaoishi katika Dahalia kwa njia ya kuwapeleka Futari kwenye Maskuli yao kuwasaidia kukidhi mahitaji yao hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
Mhe. Hemed amesema Serikali itaendelea kulipa Kipao mbele suala la Elimu kwa kuimarisha Miundombinu ya Elimu pamoja na kuimarisha Mikopo ya Elimu ya Juu kwa Wanafunzi wanaojiunga na Vyuo Vikuu kwa lengo la kuhakikisha Zanzibar inapata matokeo Mazuri pamoja na kuzalisha Wataalamu wenye uweledi katika kada mbali mbali.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed mussa amesema kuwa serikali itaendelea kutoa misaada kwa wanafunzi kwa lengo la kuwaondolea matatizo wanayokumbana nayo wakiwa skuli hasa wanafuzi waoishi katika dahalia na kumshukuru Makamu wa Pili wa Rais kwa Msaada alioutoa kwa Wanafunzi ha.
Akitoa shukrani kwaniaba ya Wanafunzi wenzake Mwanafunzi Omar Mohammed Shaali Skuli ya Sekondari ya Fidel Castro ameishukuru Serikali kwa kuwawekea Miundombinu Mizuri ya kujifunzia na kuwapatia msaada huo .
Miongoni mwa Skuli zilizopatiwa Ftari hio ni pamoja na Skuli ya Madungu Sekondari,Fidel Castro, Chuo cha Kiislamu Kiuyu, Dkt. Amani Micheweni, Idrisa Abdulwakili Kizimbani, Utaani, Wete Sekondari pamoja na kituo cha kulelea Yatima Micheweni Pemba.
Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amekabidhi Futari kwa Wafanyakazi wa Kitengo cha uratibu wa shuhuli za Chama cha Mapinduzi, Viongozi na Watendaji wa chama hicho katika Mikoa miwili ya Kichama.