VIFO VYA WALIOKULA KASA WIZARA YA AFYA YATOA RIPOTI

RIPOTI YA KASA

    Wizara ya Afya Zanzibar imetoa Ripoti ya Utafiti uliofanywa kufuatia Watoto Tisa 9 kufariki Dunia na wengine wakiendelea kupatiwa Matibabu baada ya kusadikiwa Kula Nyama ya Kasa ambayo imesababisha madhara makubwa

    Akitoa Ufafanuzi wa Rripoti hio Naibu Waziri Wizara ya Afya Hassan Khamis Hafidh amesema Tukio hilo limeripotiwa Marchi 6 katika Kijiji cha Kisiwa Panza Mkoa wa Kusini Pemba  na Watu wengine Takriban 160 wameathirika na Nyama hiyo na kupatiwa Matibabu, 

     Akitoa Taarifa ya Kitaalamu Mkemia Mkuu wa Serikali Ndg.Faridi Mpatani amesema kufuatia uchunguzi wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Bara Ripoti imebaini kuwepo kwa aina ya Sumu iliyopatikana katika Sample zote zilizokusanywa katika tukio hilo

    Naibu Mkurugenzi Kinga na Elimu ya AfyaNdg.Fatma Kabole amesema Wizara bado inaendelea kutoa Elimu pamoja na kufuatilia Wagonjwa ili kuhakikisha Wahanga wa madhara hayo wanapatiwa Matibabu

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.