Wananchi wa Jimbo la Mtambile Wilaya ya Mkoani wametakiwa kuunga mkono juhudi za Serekali katika mapambano dhidi ya uharibifu wa mazingira kwa lengo la kuepuka athari za mabadiliko ya Tabianchi.
Mbunge wa Jimbo la Mtambile Mhe.Seif Sloom sSeif ameyasema hayo katika hafla ya yakukabidhi majiko ya gesi kwa Wananchi Mia mbili Jimboni kwake, hafla hiyo iliyofanyika katika Banda la kununulia Karafuu lilipo Mtambile.
Mara baada ya kukabidhiwa majiko hayo Masheha na Madiwani, wamewataka wanufaika wa msaada huo, kutumia kwa kuzingatia
malengo yaliyokusudiwa.
Nao baadhi ya Wananchi walionufaika na majiko hayo, wamemshukuru Mbunge huyo kwa kuendelea kuwathamini Wananchi
wake, na kuwapuguzia matumizi ya kuni hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuingia hivi karibuni