Waziri Mkuu wa Serekali ya Jamuhuri ya Muungano Mhe.Kassim Majaliwa amesema Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha utaratibu wa malipo ya Wananchi waliohamishwa eneo la Nyantwali ili kupisha hifadhi na Mapito ya Wanyama.
Akijibu swali kati Bunge la Jamuhuri ya Muungano lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Ndg.Robert Maboto kuhusu malipo ya fidia kwa Wakazi wa Nyatwali katika Mkutano wa hadhara amesema kumejitokeza tatizo katika baadhi ya maeneo ambayo Wananchi wakitakiwa kulipwa fidia kwani baadhi yao wamekuwa si waaminifu kwa kuleta taarifa zisizo sahihi na wengine kuweka pingamizi juu ya utaratibu wa malipo.
Mapema Waziri Mkuu amezindua mradi wa Maji wa Misisi – Zanzibar ulioko kata ya sazira ambao umegharimu sh. milioni 733 na hadi kufikia januari, 2024 unahudumia wakazi 152,708 wa Mjini bunda.
Akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Bunda (Buwssa), Bi. Esther Gilyoma amesema mradi huo umetokana na kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa chujio la kutibu na kusafisha maji nyabehu ikiwa ni sehemu ya upanuzi wa mtandao wa huduma hiyo kuweza kuwafikia Wananchi wengi zaidi.
Kazi ya ujenzi huo ilihusisha Tanki la maji lenye ujazo wa lita 100,000 na maji hayo yanahudumia Mitaa ya Nyasura ‘b’, Zanzibar na Misisi Mjini Bunda.