MHE. SHARIF, AMEWATAKA WATENDAJI KUWEKA KUMBUKUMBU

MHE. SHARIFF ALI SHARIFF

Waziri wa Afisi ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe Shariff Ali Shariff  amewataka Watendaji wa Taasisi hiyo kuweka kumbukumbu katika Utendaji wao wa kazi ili kuonesha hatua iliyofikiwa katika kazi zao.

Ameyasema hayo mara baada ya kukabidhiwa Afisi ya Rais, kazi Uchumi na Uwekezaji na aliyekuwa Waziri wa Afisi hiyo Mhe Mudrki Ramadhani soraga.

Mhe Shariff amewaomba Watendaji wa Ofisi hyo kuwa na ushirikiano katika kazi ili kuendeleza kazi nzuri wanazozifanya.

Waziri wa Utalii na  Mambo ya Kale Mhe Mudrki Ramadhani soraga amewataka watendaji wa afisi hiyo kuwajibika katika majukumu yao pamoja na kuendeleza ushirikiano kwa Viongozi wao ili kufanya kazi kwa ufanisi.

Katibu Mkuu Afisi ya Rais Kazi, Uchumi na uwekezaji Dr Habiba Hassan  Omar ameahidi kutekeleza yale yote mazuri kwa Viongozi wao kwa kutoa ushirikiano katika kazi zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.