UNICEF YASAIDIA SEKTA ZA AFYA, ELIMU NA WATOTO ZANZIBAR

Waziri Haroun na Unicef

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman amesema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto Duniani  (UNICEF) limekuwa na msaada kwa Zanzibar katika Sekta mbalimbali ikiwemo ya Afya, Elimu pamoja na haki za Watoto.

    Akizungumza na Mwakilishi Mkaazi wa Unicef Tanzania Ndg.Elke Wishes huko Mazizini ameliomba Shirika hilo kuendelea kuisadia Zanzibar ikiwa ni pamoja na kusaidia Vifaa vya kisasa vya kuwawezesha Watoto kuwarahisi kusikilizwa Mashauri yao katika Mahakama ya Watoto Mahonda.

    Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kusaidia Watoto Nchini Tanzania Elke Wish ameahidi kufanya ziara pamoja na Waziri wa Sheria wa Canada na kuona jinsi gani wataweza kusaidia Mahakama hiyo na maeneo mengine Zanzibar.

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.