Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala bora Mhe Harouna Ali Suleiman amezitaka Madrasa za Dini kusimamia misingi ya Kiislam ili kutokomeza vizendo vya uhalifu.
Akifunga Mafunzo ya Walimu wa Madrasa ya Elimu ya Amali Waziri Haroun amesema misingi ya Dini iliyobora humjenga Mwanafunzi kuwa na Muongozo mwema katika Uislamu hivyo ni vyema kuhakikisha Mafunzo hayo yanaleta tija kwa Walimu.
Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Zanzibar Khalid Ali Mfaume amewaomba Walimu wa Madrasa ya Elimu ya Amali kupinga Vitendo vya ukatili wa Kijinsia kwa Wanafunzi ili kuweza kuvitokomeza Vitendo hivyo.
Akisoma Risala Mwanafunzi wa Madrasa hiyo Maryam Ramadhan amesema Licha ya ufinyu wa Jengo bado wameweza kupatiwa Taaluma mbalimbali hvyo wameomba kupatiwa sehemu ambayo itakayo kidhi kuendelea na Masomo yao