Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imesema inaendelea kufanya Mageuzi katika Sekta ya Elimu ili kuona Wanafunzi wanapata Elimu iliyo bora.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt .Mwanahamisi Adam Ameir amesema hayo alipokuwa akifungua Maonyesho ya kazi za Mikono zilizofanywa na Wanafunzi wa Skuli ya Ben Bela katika hafla ya kutimiza Miaka 100 ya Skuli hiyo , Amesema Sekta ya Elimu ina mchango mkubwa kwa Jamii hivyo ni muhimu kutoa Elimu iliyobora kwa Wanafunzi ambayo itaweza kuwasaidia kutoa Wanafunzi Mahiri .
Amefahamisha kuwa kazi za mikono zinazofanywa na Wanafunzi zitaweza kuwasaidia wanapomaliza Elimu ya Sekondari na Vyuo Vikuu kwa kujiajiri wenyewe.
Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Wasichana Benbela Ndg. Zainab Mbwana Mgunda amesema Sera ya Elimu inaelekeza Wanafunzi wasome masomo ya vitendo ili wawe na ujuzi utakaowasaidia baada ya kumaliza Masomo yao.