Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dk.Philip Isdor Mpango amesema ili kuhakikisha Tanzania inaendana na mabadiliko ya huduma za Afya imejipanga kuwekeza kupitia Hospitali zake.
Akifungua Mkutano wa Madaktari Bingwa wa moyo Afrika amesema mpango huo umezingatia zaidi kuwa na vifaa vya kisasa na kusomesha Madaktari wake kwa idadi kubwa ili kutosheleza katika kuwafikia Wananchi.
Amesema Magonjwa ya moyo yamekuwa yakiongezeka na kuchangia vifo vingi hivyo Serikali imeona kuna kila sababu za kuimarisha Taasisi hizo pamoja na Hospitali zake Nchini ili kupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
Waziri wa Afya Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe.Ummi Ali Mwalim na Naibu Waziri wa Afya Zanziba Mhe.Hassan Khamis Hafidh wamewahimiza Wananchi kufuata ushauri wa Madaktari katika kuacha matumizi ya Pombe na kuzingatia ulaji wa vyakula ili kuepuka Magonjwa ya moyo na figo ambayo yamekuwa na gharama kubwa katika Matibabu yake.
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dk. Peter Richard Kisenge amesema ukubwa wa tatizo la Ugonjwa huo umepelekea Serikali kuanzisha Taasisi hiyo ambayo ni mfano kwa Afrika Mashariki katika kutoa huduma bora
Mkutano huo wa Pili kufanyika umeshirikisha zaidi ya Wataalamu mia tano kutoka Mataifa mbali mbalimbali na miongoni mwa mada watakazojadili ni namna ya kujikinga na Ugonjwa wa Moyo