ZURA YATAJA SABABU YA ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA

ZURA

   Mamlaka ya udhibiti huduma za Maji na Nishati Zanzibar ZURA imetangaza kuongezeka kwa Bei za Mafuta kwa Mwezi wa February 2024 zitakazoanza kutumia Ijumaa ya Wiki hii.

    Akitangaza Bei hizo kwa Waandishi wa Habari Meneja Kitengo cha Uhusiano ZURA Ndg.Mbarak Hassan Haji amesema kupanda kwa bei hiyo kunatokana na kuongezeka kwa gharama ya uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es salama na Tanga

   Amesema Mamlaka hupanga Wastani wa Bei kutokana na mwenendo wa mabadiliko ya bei za Mafuta Duniani, Thamani ya Shiling ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani, gharama za Usafiri na Bima  hadi Zanzibar pamoja na kodi za Serikali kwa kiwango cha faida kwa Wauzaji wa jumla na reja reja.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.