JAMII IMEHIMIZWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA

MKURUGENZI MKUU ZBC

Jamii imehimizwa kuunga Mkono juhudi za Serikali za kuimarisha Sekta ya Afya kwa kujitokeza kuchangia Damu salama ili kupunguza idadi ya Vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.

Akifungua Kampeni ya kuchangia Damu salama Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la utangazaji Zanzibar ZBC Ramadhan Bukini amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza idadi kubwa ya vifo vya Wakinamama hao ambao wamekuwa wakipungukiwa na Damu wakati wa kujifungua na kusababisha kupoteza Maisha yao.

Meneja Masoko na kuendeleza Biashara Benki ya Watu Zanzibar  PBZ  Seif Suleyman Mohamed amesema  suala la ukusanyaji wa Damu salama ni jambo muhimu kwa Jamii kwani huimarisha Afya za Wananchi na kusababisha kukuza Uchumia wa Taifa.

Meneja Mpango wa Damu salama Zanzibar Masoud Ali Masoud amesema wanashirikiana na Wadau mbalimbali kuanzisha Mabonanza ambayo yataifanya Jamii kushiriki kwa wingi kuchangia Damu ili kuokoa maisha kwa wenye uhitaji.

Wadau walioshiriki Kampeni hiyo wamesema wataendelea kuunga Mkono juhudi zilizoanzishwa za kuimarisha kuchangia Damu Salama na kutoa wito kwa Jamii kujitokeza kwa wingi ili kufikia malengo.

Kampeni ya Mwamvuli wa Damu Salama inatarajia kukusanya zaidi ya mifuko 250 ambayo  imeandaliwa na Shirika la Utangazaji Zanzibar  ZBC, na kuwashirikisha Wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya PBZ, Al - Sadik .Foundation, Zanzibar School of Health, Tigo Zantel ,ZRA na Hospitali ya Arahma.                       

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.