ZAECA KUFANYA UCHUNGUZI DHIDI YA WAFANYAKAZI WA MKATABA

MHE. SHAABANI ALI  OTHMAN

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Shaabani Ali Othmani ameitaka Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa kufanya uchunguzi dhidi ya Wafanyakazi wa Mkataba ambao walikuwa wanaohusika na ukusanyaji wa Mapato katika hifadhi za Chabamca  kutokana na kupoteza kwa mapato katika maeneo hayo.

Agizo hilo amelitoa alipozungumza na Wakuu wa Taasisi wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi pamoja na Watendaji wa Vituo vya hifadhi ya Chabamca huko Maisara amesema kwa muda mrefu Serikali imekuwa ikihimiza wakuu wa Taasisi kukusanya mapato na kudhibiti uvujaji wa mapato lakini maeneo hayo bado kuna mianya unaotumika kuvujisha mapato.

Mkurugenzi uchunguzi na Opereshen Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa (ZAECA) Nassor Ahmed Haji ameahidi kuhakikisha Wanafanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa aliyehusika.

Wafanyakazi waliosimamishwa Kazi ni pamoja na Maofisa mapato kutoka hifadhi za Chabamca ikiwemo Mizingani, Jitini, Forodha Mchanga AFrica house na Prison Island.

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.