Wananchi wamehimizwa kuthamini kazi zinazofanywa na watafiti zinalenga kuendeleza utalii wa mazingira juwa endelevu ili zanzibar kuwa kivutio cha wageni na wakaazi wake.
Akifungua Mafunzo ya kuwasilisha Matokeo ya Utafiti wa Mazingira yanaweza kuimarisha utalii nchini huko katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Maruhubi Naibu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Dkt. Hashim Hamza Chande, amesema utafiti kuwashirikisha Wananchi katika Maeneo yao kutatoa msukumo wa utekelezaji wa matokeo hayo na kupata suluhisho la kudumu. amesema kuwa utafiti huo umetoa muongozo wa namna ya kujikinga na Mbu kwa njia salama bila kutumia Kemikali ambao kwa sehemu kubwa wanazalishwa katika taka na sehemu nyengine zenye uchafu.
Dkt. Hashim amesema kuwa utafiti huo unakwenda sambamba na malengo ya Dira ya 2050 ya uhifadhi wa mazingira ambao unao uhusiano mkubwa baina ya Wawekezaji, Wasimamizi kwenye Hoteli pamoja na Jamii kusimamia Ustawi wa Mazingira
Wakiwasilisha matokeo ya Utafiti Mkurugenzi Msimamzi wa shughuli za Utalii, Ndg. Adil George wa Kamisheni ya Utalii akiwasilisha Kampeni ya Kijani Zanzibar amesema Hoteli za Kitalii zinazalisha Asilimia 60 ya taka zitaweza kutumika kwa matumizi mengine.
Sheha wa Shehia ya Nungwi Bandakuu Ndg.Haji Khamis Haji alikiri kuwa tangu ulipoanzishwa utafiti wameshirikishwa
Mafunzo ya kujenga uelewa kuhusiana na utafiti huo yanatolewa katika Kijiji cha Michamvi, Paje na Nungwi kwa ushirikiano na Masheha na Viongozi wa Wilaya.