Zaidi ya Wananchi 103 wa Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani wameanza kutumia Umeme wa ZECO baada ya Nyumba zao Shirika kukamilisha utaratibu.
Akizungumza na ZBC, Afisa Mawasiliano na huduma kwa Wateja Shirika la Umeme Zanzibar Tawi la Pemba (ZECO), Ndg.Haji Khatib Haji amesema baada ya Wananchi kupatiwa Elimu na kushajiliwa tayari Wananchi 103 wameanza kunufaika na huduma hiyo.
Amesema Wananchi wataweza kunufaika na Umeme kwa ajili ya kusomea muda wa ziada, kuhifadhi samaki wao ikizingatiwa
Wananchi wa Kisiwa Panza shughuli zao kuu ni Uvuvi.
Nae Sheha wa Shehia ya Kisiwa Panza Ndg.Haji Ali Shaali, ameishukuru ZECO kwa kuwahamasiha wananchi na kuhamaisika. Jumla ya wananchi 103 wamesajiliwa ili kuungiwa huduma ya Umeme.
Nao baadhi ya Wananchi walioungiwa huduma hiyo, walikua na haya kueleza furaha zao baada ya kuuingiwa huduma ya Umeme.
Kisiwa Panza kipo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, ni moja ya Visiwa vidogo vidogo vinavyopatikana ndani ya Kisiwa cha
Pemba.