Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda, ameagiza ununuzi wa Mazao ufanyike kwa Soko huria, na siyo stakabadhi Ghalani.
Ametoa agizo hilo katika Mkutano wa hadhara Mjini Bariadi, baada ya kupokea ombi la Mbunge wa Jimbo la Bariadi, Mhandisi kundo Andrea Mathew, aliyeomba ununuzi wa mazao yakiwemo choroko, Mbaazi na mengineyo yafanyike katika Soko huria ili kumnufaisha Mkulima.
Mbunge wa Jimbo la bariadi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Mhandisi kundo Andrea Mathew, amesema ununuzi wa Mazao kwa njia ya stakabadhi Ghalani kupitia AMCCOS unaweza kudhoofisha ushindani wa bei ya Soko la Mazao.
Katika Mkutano huo Makonda amepongezwa na Watemi wa mila la Kisukuma na kupewa Jina la Bagololage, yaani 'WANYOOSHE.'