Kamisheni ya wakfu na mali ya amana Zanzibar imetoa sadaka ya nyama iliyotoka Saudi Arabia kwa wakuu wa wilaya wa Unguja na Pemba ili kuwapatia wananchi wasiojiweza .
Akikabidhi sadaka hiyo kaimu mkuu wa Divisheni ya zaka na misaada kamisheni ya wakfu na mali ya amana Zanzibar Ndg. Hassan Ali Kombo kwa niaba ya katibu mtendaji amesema watahakikisha sadaka hiyo inawafikia waliokusudiwa ikiwemo watu wenyemahitaji maalum , na taasisi za kulelea watoto yatima .
Nao wananchi waliopatiwa sadaka hiyo wamesema wamefarajika kwa kupatiwa sadaka hiyo na kuwaomba viongozi kuendelea kuwasaidia kwa kupatiwa misaada ili kujiendeleza kimaisha.
stories
standard