ZBS WATAKIWA KUENDELEA KUZINGATIA VIWANGO VYA BIDHAA NCHINI

KAMATI BARAZA LA WAWAKILISHI NA ZBS

  Kamati ya Utalii Biashara na kilimo ya baraza la wawakilishi imeitaka Taasisi ya viwango Zanzibar ZBS kuendelea kuzingatia viwanzgo vya bidhaa nchini ili kusaidia Serikali kudhibiti bidhaa zilizokwisha wa muda wa matumizi kuingizwa nchini .

    Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara ya kamati ya utalii , biashara na kilimo ya Baraza la wawakilishi makamo mweyeketi wa kamati hiyo Mh. Hussein Ibrahim Makungu , amaesma taasisi hiyo ina umuhimu kwa serikali na kubaini matatizo na kutafutia ufumbuzi ili kuwafanya wannchi kubaki salama.

    Mkurugenzi mkuu wa ZBS Ndg. Yussuf Majid Nassor akiwasilisha ripoti ya miezi sita amesema wamepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kudhibiti  bidhaa na viwango vya biashara kwa watumiaji , kuongeza maabara na kuendelea na kutanua wigo wa kujitangaza kwa taasisi hiyo.

    Wakichangia ripoti hiyo Wajumbe wa kamati hiyo , wamesema Taasisi hiyo ni muhimu kwa jamii kwani imekuwa ikilinda afaya za wananchi na kuwashauri ZBS kufanya  ziara za mara kwa mara katika maduka ya bidhaa ili kudhibiti bidhaa zilizokwisha muda  wa matumizi yake.

   Taasisi ya viwango Zanzibar ZBS inahitaji wataalamu  na wafanyakazi wa kutosha ili iweze kujiendesha wenyewe.

 

 

 

 

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.