Wananchi Wilayani Handeni Mkoani Tanga wamelalamika kukosa huduma ya umeme wa uhakika kwa kukatika mara kwa mara, huku wakiliomba shirirka la umeme Tanzania (TANESCO) kutoa taarifa kwa uwepo wa tatizo hilo .
Wakizungumza kwenye kikao maalum kilichoitishwa na uongozi wa kata ya Chanika Wilayani hapa , Wananchi hao wamesema kuwa imefika hatua hata vifaa vyao vya ndani vinaungua kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara.
Meneja wa Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Handeni Ndg. Mussa Chowo akijibu kuhusu changamoto hiyo amekiri ni kweli kuna tatizo la kukatika umeme Wilayani humo, ila zipo sababu ya kutokea tatizo hilo.
Mwenyekti kamati ya huduma za jamii halmashauri ya Mji wa Handeni na Diwani kata ya Chanika ndg.Abdallah Chihumpu amesema ni kweli hali ya umeme sio nzuri kabisa katika kijiji chao , kwani umekuwa ukikatika na wakati mwingine taarifa kwa wateja hazifiki kwa wakati.
Serikali ipo kwenye mchakato wa kuweka kituo cha kupooza umeme mkata kuelekea Handeni Mjini ,kwa lengo la kupata huduma ya umeme ambao hautegemewi na wilaya nyengine ,kitendo kinachosababisha kutokea kwa tatizo hilo.