MFUKO WA MAAFA KUWEZESHWA ILI KUKABILIANA NA MAAFA YANAPOTOKEA.

NAIBU KATIBU MKUU WA OFISI YA MAKAMO WA PILI

Kamati ya kudumu ya kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi imeishauri ofisi za Makamu wa pili ya Rais kupitia Kamisheni ya kukabiliana na Maafa kuaandaa utaratibu wa kuupatia fedha Mfuko wa kukabiliana na Maafa ili yanapotokea maafa Serikali iwe na uwezo wa kuwasaidia Wananchi wake kupitia Mfuko huo.

Ushauri  huo umetolewa  na Wajumbe  wa Kamati ya kudumu ya kusimamia Ofisi za  Viongozi Wakuu wa Kitaifa Chini ya Mwenyekiti wake Mh.Maryam Thain Juma mara baada ya kupokea  Taarifa ya utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha robo ya pili Oktoba –Disemba kwa Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais huko katika Ukumbi wa Ofisi hiyo Tibirizi.

Pia kamati hiyo imeishukuru Ofisi ya Makamo wa Pili ya Raisi kwa Mashirikiano wanayoyaonyesha kwa  Wafanya kazi na Viongozi  pamoja na usimamiaji mzuri wa Miradi  mbali mbali ikiwemo Miradi ya TASSAF.

Akisoma Taarifa  ,Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Salhina Mwita Ameir amesema  Ofisi hiyo imepata mafanikio makubwa ikiwemo ya kuimarisha hali za kiuchumi za Walengwa wa Tassaf kupitia Mpango wa kunusuru Kaya Masikini na kuongezeka kwa fursa za ajira kwa Walengwa waliyopatiwa fedha za  ruzuku ya uzalishaji.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.