Hayo Yameelezwa Na Wajumbe Wa Kamati Ya Mawasilianio, Ardhi Na Nishati Ya Baraza La Wawakilishi, Chini Ya Makamo Mwenyekiti Wake Mhe Azza Januar Joseph, Wameyaeleza Hayo Wakati Walipotembea Miradi Mbali Mbali Ya Maji Na Kupokea Taarifa Ya Utekelezaji Wa Bajeti Ya Mamlaka Ya Maji Zanzibar (ZAWA) Kwa Kipindi Cha Julai Hadi Disemba 2023 .
Wameilekeza Wizara Ya Maji Kuhakikisha Inaendelea Kuisimamia Kwa Karibu Ujenzi Wa Miradi Hiyo Nchini Kote Ili Miradi Mingi Itekelezwe Kwa Ubora Na Kukamilika Kwa Wakati Na Hatimae Dhamira Ya Serikali Itimie Kikamilifu.
Nae Mkurugenzi Mkuu Wa Mamlaka Ya Maji Zanzibar (ZAWA) Mhandisi Dr Salha Mohammed Kassim, Ameihakikishia Kamati Kwamba Wataendelea Kupambana Muda Wote Kuhakikisha Wananchi Wanaendelea Kupata Huduma Ya Maji Safi Na Salama Na Yenye Kutosheleza Ili Kuweza Kupunguza Adha Ya Ukosekanaji Wa Wa Huduma Hiyo Iliyokuwepo Katika Baadhi Ya Maeneo.