Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema Chuo Cha Afya Cha Zanzibar School Of Health ni moja ya Matunda ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuhakikisha Wananchi wake wanapata huduma za afya zilizo bora.
Akizungumza katika Mahafali ya 11 ya Wanafunzi wa Chuo hicho amesema katika Sekta ya afya bado kuna pengo kubwa la Wataalamu hivyo Chuo hicho kinawajibu wa kuzalisha Wataalamu ambao watatoa huduma kwa Jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar School of Health Aziza Hamed amesema Zanzibar School of Health inadhamiria kuchangia kuwandaa Vijana ili kutoa huduma za Afya na kujiajiri.
Naibu Waziri wa Elimu Zanzibar Mhe, Ali Abdul-ghulam Hussein amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi Binafsi katika maendeleo.
Jumla ya Wahitimu Miatano ishirini na sita wamehitimu na kutunukiwa Vyeti