Kampuni Za Wakandarasi Wazawa Zinazoendelea Na Matengenezo Ya Barabara Za Kiwango Cha Changarawe Katika Halmashauri Za Buchosa, Sengerema Na Ukerwe Ni Sita, Ambazo Ni Lean Engineers Ltd Ya Dar Es Salaam, Samota Ya Nzega, Jonta Investment Ltd Ya Shinyanga, Am & Partner Ltd Ya Dar Es Salaam, Kasco Ltd Ya Mwanza Na Cym Contractors Ltd Ya Singida.
Meneja Wa Tanroads Mkoa Wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose Amesema Matengenezo Ya Barabara Hizo Zenye Urefu Wa Kilometa Zaidi Ya Mia Tatu Yanatarajia Kukamilika Kabla Ya Juni 30 Mwaka Huu.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Kampuni Ya Lean Engineers Ltd Inayojenga Barabara Yenye Urefu Wa Kilometa Tisini Katikawilaya Ya Ukerewe Mhandisi Zakaria Mshandete, Amesema Matengenezo Ya Barabara Hiyo Yatakamilika Ndani Ya Muda Usiozidi Miezi Mitatu.
Diwani Wa Kata Ya Murutunguru Nicholaus Mnyoro Mbali Na Kumpongeza Mkandarasi Wa Barabara Hiyo, Amesema Kukamilika Kwa Barabara Hiyo Kwa Wakati Kutafungua Fursa Nyingi Za Kiuchumi Kwa Wananchi Wa Ukerewe.
Baadhi Ya Watumiaji Wa Vyombo Vya Moto Wakiwemo Wakazi Wa Vijiji Inakopita Barabara Hiyo Wameishukuru Serikali Kwa Kuifanyia Matengenezo Barabara Hiyo Ambayo Kwa Muda Mrefu Ilikuwa Ikipitika Kwa Shida.