Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amejumuika pamoja na Viongozi wa jumuiya ya umoja wa Vijana UVCCM katika hafla ya Chakula cha usiku
Akizungumza na Vijana katika hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi amesema
Serikali na Chama cha Mapinduzi wamefarajika kwa kuungwa mkono katika sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya
Zanzibar.
Amesema anaridhishwa kuona Vijana wa umoja wa Vijana (UVCCM) wanaunga mkono katika sherehe za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
Akitoa shukrani kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Taifa, Mohamed Ali kawaida amesema vijana wametembea kwa Miguu Nchi nzima kwa maana Unguja na Pemba jambo ambalo limewapa ari kwa utendaji mzuri wa kazi na kulitumikia Taifa.