Serikali imesema itaendelea kuweka Mazingira wezeshi ya uwekezaji wa Kitanzania ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC ikiwemo punguzo la asilimia 75 kwenye Vifaa vinavyotumika katika uwekezaji
Kauli hiyo imesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha uwekezaji Tanzania [TIC] Gilead Teri alipotembelea wawekezaji Jijini mwanza ndipo akaona ipo haja ya kuwawekea mazingira wezeshi ili wafanye shughuli zao kwa ufanisi
Patrick Kalangwa ni Katibu Tawala Msaidizi Viwanda biashara na uwekezaji Mkoa wa Mwanza amesema kwa kushirikiana na Wizara watahakikisha wawekezaji wanapata mikopo yenye Riba nafuu huku mwekezaji wa Nyama John Chobo akisema atawaelekeza wawekezaji wenzake kufuga kisasa
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amos Makalla amesema atashirikiana na TIC katika kuhakikisha wawekezaji wanapata urahisi wa kufanya shughuli zao.