UWEKEZAJI WA MIRADI YA NYUMBA ZA MAKAAZI KWA WAGENI, UMEKUWA NI WA PILI KWA KULETA MITAJI MIKUBWA HAPA NCHINI.

makamo wa kwanza

Ameyasema hayo Makamo Wa Kwanza Wa Rais Wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Katika Uzinduzi Wa Mradi Wa Nyumba CPS The Soul Huko Paje, Amesema Hatua Hiyo Itasaidia Kuitangaza Zanzibar Na Kushajihisha Wageni Kuingia Nchini Na Kutembelea Vivutio Vilivyomo.

Amesema Uwekezaji Huo Unaochukuwa Nafasi Ya Pili Badala Ya Hoteli Za Kitalii Utawahakikishia Hifadhi Za Malazi Na Usalama , Ambapo Serikali Inaendelea

Kuimarisha Sera Na Sheria Ili Kutanua Zaidi Shughuli Za Uwekezaji.

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais ,Kazi Uchumi Na Uwekezaji Mh Mudrik Ramadhan Soraga, Ameiomba Serikali Ya Mkoa Kuendelea Kusimamia Mpango Wa Matumizi Ya Ardhi Ili Kuwa Na Ardhi Ya Akiba Kwa Ajili Ya Miradi Zaidi

Kwa Upande Wake, Mkurugenzi Wa Mamlaka Ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar Zipa Shariff Ali Shariff, Amesema Wataongeza Nguvu Katika Kusimamia Miradi Inayoanzishwa Kwa Lengo La Kulinda Mazingira Ya Maeneo Hayo.

Nae Mkurugenzi Kampuni Ya CPS Thobias Dietzold, Amesema  Miradi Ya Nyumba Imeonesha Kukua Zaidi Kutokana Na Miongozo Bora Ya Serikali Na Kuleta Manufaa Makubwa Kwao Na Serikali.

Mradi Wa The Soul Of Zanzibar Villa Una Nyumba Zaidi Ya Mia Mbili Na Hoteli Ambapo Hadi Kukamilika Kwake Utagharimu Zaidi Ya Shilingi Bilioni 50 Na Kutoa Ajira 50 Za Vijana.

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.