Man U wanachunguzwa kwa kuwapa mashabiki nyama mbichi ya kuku
Manchester United inachunguzwa na Baraza la Trafford kufuatia madai kwamba mashabiki walilishwa nyama ya kuku mbichi katika hafla iliyoandaliwa hivi majuzi huko Old Trafford.
Watu kadhaa wanadai kuwa hawakuwa sawa kufuatia tukio hilo na tukio hilo sasa linachunguzwa.
Kwa mujibu wa gazeti la Athletic, United ilipokea malalamiko kadhaa na wanafanya uchunguzi wao wa ndani
Klabu inapata mapato makubwa kutokana na kuhudumia chakula na kuandaa hafla na kupunguzwa kwa viwango vyao vya usafi kunaweza kuathiri hilo.