SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWENYE MIUNDOMBINU YA SEKTA YA ELIMU
Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya elimu ili kuwawezesha vijana kusoma fani tofauti ndani ya Nchi.
Rais wa Zanzibar ameyasema hayo katika mahafali ya 19 ya Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA na kuwatunuku vyeti, stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu kwa wahitimu wa Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2022/2023, huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.