Bodi ya Mikopo ya Elimu ya juu Zanzibar imepanga kudhamini Wanafunzi zaidi ya Elfu 7 kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025 ambapo kati yao Wanafunzi zaidi ya Elfu 4 wanaoendelea na Masomo na Wanafunzi Elfu 3 wanaoanza Masomo.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Muongozo wa Utowaji Mikopo na Mfumo wa Mikopo kwa Mwaka 2024/2025 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh.Ali Abdulghulama Hussein amesema hatua hiyo imesababisha kuongeza Bajeti ya Fedha kutoka Bilioni 29 Nukta 9 kwa Mwaka 2023 hadi Bilioni 33 Nukta 3
Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Iddi Khamis Haji amesema mbali ya udhamini kutolewa kwa Ngazi ya Shahada ya Kwanza ya Pili na ya Tatu bado Wataanza kutoa kwa mara ya Kwanza Ngazi ya diploma
Wadau wa Elimu kutoka Taasisi mbali mbali wamepongeza hatua ya Serikali kuongeza Bajeti kwa ajili ya Wanafunzi pamoja na kulipa Fedha za kujikimu kabla ya kuanza Masomo.