Zahanati hiyo iliyojengwa na TASAF kwa gharama za Shilingi Milioni 93 imekamilika ikiwa na Vifaa vyote pamoja na Dawa..
Ujenzi wa Nyumba ya kuishi Watumishi wa Afya wa Zahanati hiyo ambayo ujenzi wake umefikia Asilimia 95 na Wodi ya Wazazi nayo ikiendelea kujengwa.
Akizungumza Wakati wa Uzinduzi wa Zahanati hiyo Mwenyekiti wa Kijiji cha Bugando, Charles Methusela Kasuka amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo kutawaondelea adha ya kutembea umbali mrefu kufata huduma za Afya katika Kata za Jirani.
Mbunge wa Jimbo la Magu Mhe. Boniventura Kiswaga ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutoa Fedha za kufanikisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Wilaya ya Magu
Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Magu, Eusebius Chanjali amewataka Wananchi wa Kijiji cha Bugando kutumia Zahanati hiyo kutatua shida zao za kiafya na kutoa ushirikiano wa Watumishi wa Zahanati hiyo
Mratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Wilaya ya Magu , Daniel Samwel Sanyenge amesema Serikali imejenga Zahanati hiyo kutokana na uhitaji Mkubwa uliyopo kwa Wakazi wa Maeneo hayo ambao wanatembea umbali mrefu kwenda Kata Jirani kufata huduma za Afya. .
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Magu Mohamed Ramadhani amewaomba Wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika Ujenzi na Ulinzi wa Miradi inayojengwa na Serikali ili ilite tija iliyokusudiwa ya kutoa huduma.