Jumla ya Kadi elfu 44 Mia Tano na 95 zimetolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar kwa Watu waliojindikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza .
Akizungumza na Waandishi wa habari huko Maisara kuhusu ugawaji wa Kadi Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar Nd Thabit Idarous Faina amesema hatua hiyo imeonyesha kuwa Wananchi wana mwamko mkubwa katika kuhakikisha wanatumia haki yao ya kupiga Kura wakati utakapofika na kwamba idadi hiyo.
Amesema hatua hiyo pia itauwezesha Uchaguzi kuwa huru na haki kutokana na Wananchi hao kuwa Kadi ambazo zinatawawezesha kupiga kura.
Aidha Mkurugenzi faina amewaomba Wananchi kuhakikisha wanaandika Taarifa sahihi wakati wanapojiandikisha ili kuona wanapata Kadi zao kwa urahisi huku akiwaomba Wananchi waliokuwa hawajachukua KAdi hizo kuzifuata katika Ofisi zao za Wilaya ambapo jumla ya Kadi Elfu 13 Mia Mbili na 88 bado haziajchukuliwa.
Jumla ya Wananchi Elfu 57 Mia Nane na 83 waliandikishwa katika Daftari la kudumu la Wapiga Kura awamu ya mwanzo lililofanyika Disemba Mwaka jana hadi Januari Mwaka huu.