Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji imejipanga kuondosha tatizo la ukosefu wa Ajira Nchini kwa kuandaa Mifumo itakayoendana na matakwa ya Waajiriwa itakayowahamasisha kufanya kazi kwa Ufanisi.
Huyo ni Mhe.Sharif Ali Sharif, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji, akifungua Warsha juu ya Uaandaaji wa Mifumo ya Soko la Ajira huko Golden Tulip Waziri huyo ameuhakikishia Umma kwamba Mifumo hiyo itakapokamilika itaondosha urasimu katika Soko la Ajira.
Ndg.Hafidh Khamis Afisa Programu Shirika la Kazi Duniani, amesema Shirika hilo litaendelea kusaidiana na Wizara ya Kazi kufanikisha Mfumo huo.
Warsha hiyo ya Siku 4 imeandaliwa na Shirika la Kazi Duniani ilo ikishirikiana na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji.