WAZIRI MCHENGERWA AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

WAZIRI MCHENGERWA

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi Mhe.Mohamed Mchengerwa ,amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wilaya  kusikiliza  Kero za Wananchi waliopo kwenye Vijiji, Mitaa na Vitongoji. 

    Waziri  Mchengerwa ametoa Maagizo hayo Jijini Dodoma Wakati Akizindua Programu ya uimarishaji wa Tawala za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.

    Aidha  ameongeza kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia Programu za maboresho ya Serikali za Mitaa tathmini mbalimbali zimebaini kuwepo kwa Changamoto zikiwemo muingiliano wa Majukumu katika Utoaji wa huduma za Kiuchumi na Kijamii baina ya Wizara za Kisekta na Mamlaka za Serikali za Mitaa

    Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Denis Londo, amesema Programu hiyo itaenda kutatua changamoto kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa na kuibua vyanzo vipya vya Mapato.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.