Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja inawashikilia Watu Wawili kwa tuhuma za kutaka kuiba Mafuta kwenye Gari ya Miradi ya Ujenzi wa Barabara katika Bandari ya Mwangapwani.
Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo huko Mahonda Kamanda wa Polisi Mkoa huo Kamishna Msaidizi wa Polisi Daniel Shila amesema Jeshi hilo lkiwa katika Doria zake huko eneo la Kitope kwenye Maegesho ya Gari ya Kampuni ya Orkun, limewakamata Watu hao wakiwa na Madumu na Mipira ya kunyonyea Mafuta kwa nia ya kutaka kuiba Mafuta.
Aidha katika tukio jengine Jeshi hilo pia limemkamata Mtu mmoja kwa tuhuma za Wizi wa Pikipiki mbili.
Wakati huo huo Kamanda Shila amekagua utendaji kazi wa Askari Polisi katika Mkoa huo na kuwataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi hilo kufanya kazi na kuzingatia Nidhamu, Weledi na Uwadilifu.