Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewataka Watendaji kuzifanyia kazi sheria mpya zilizotiwa saini kwa kwa maslahi ya Wananchi.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa Sheria nne zikiwemo Sheria ya huduma ndogo za Fedha, sheria ya Mahakama ya Kadhi Mkuu Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar 2023, na Sheria ya Ukaguzi wa Uma katika Viwanja vya Ikulu Mjini Zanzibar, Dr Mwinyi amesema hatua hiyo ya kusaini hadharani sheria hizo ni ya kihistoria na kuweka uwazi na kufahamu yaliomo ndani ya sheria hizo.
Aidha Dkt. Mwinyi amewakumbusha Wawekezaji kutimiza wajibu wao na kusimamia haki ili kazi ziweze kuwa na tija inayotakiwa.
Amesema Serikali ya awamu ya 8 imeweka mkazo uchumi wa buluu na kutoa wito kuchukua hatua ya kuzipitia sheria ambazo zinakwaza katika utekelezaji wa Wananchi
Wakitolea ufafanuzi baadhi ya sheria hizo Mawaziri hao wamesema sheria hizo zitasaidia kukuwepo ukweli na uwazi katika utekelezaji wa kazi zao.