Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Khamis Ramadhan Shaaban amewataka Watendaji wa Mahkama kufanya kazi kwa ushirikiano ili kudoa migogoro baina yao na Wananchi.
Ameyasema hayo katika ziara ya kila Mwaka ya kuzitembelea Mahkama Jaji Khamis amesema ni vyema kuwa na ushirikiano bora ili kuondokana na vitendo vya rushwa ambavyo vitaleta ufanisi katika kazi.
Mrajis wa Mahkama kuu Mhe Valentina Adrew Katema amewasisitiza Wafanyakazi hao kuhakikisha mienendo ya kesi inafatiliwa kwa umakini ili Wananchi Wajenge imani na Mahkama zao.
Wafanyakazi wa Mahakama wameelezea matatizo wanayokabiliana nayo ikiwemo vitendea kazi ili kuzidi kufanya kazi kwa ufanisi.
Ziara hiyo ya Jaji Mkuu ambayo ametembelea Mahkama za Mkoa wa Kusini Unguja na ujenzi wa Jengo la Mahkama ya Mkoa wa Kusini liliopo Binguni.