Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Doto Biteko amesema wakati umefika kwa Vijana kujifunza kutoka kwa Wazee ili kuwa Wazalendo wa Nchi yao.
Akizungumza katika Kongamano la kuadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Biteko amesema ni vyema kwa Vijana hao kuwa Mstari wa mbele katika kufanikisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuna baadhi ya Watu ambao Siasa zao ni za ushindani zinazosababisha kufanywa uzungumzwe kwa mtazamo tofauti hivyo kutokubali kuvyunjwa Moyo na kusonga mbele Kimaaendeleo.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi UVCCM Taifa Muhamedi kawaida amesema Kongamano hilo la Miaka 60 ya Mapinduzi litaleta chachu kwa Vijana kuijuwa historia ya CCM ili kuhakikisha waleta maendeleo ndani ya umoja huo.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashidi Simai Msaraka amesema Vijana wamekuwa Dira wa Taifa na ndio wanaoshika nafasi mbali katika chama na matumaini makubwa ili kuongeza Uwaminifu kwa ufanisi .