WAJASIRIAMALI JIMBO LA UZINI WAOMBA KUPATIWA MITAJI

WAJASIRAMALI  WANAWAKE JIMBO LA UZINI

   Zaidi ya vikundi 13  vya wajasiriamali wanawake katika Jimbo la Uzini wamewaomba viongozi wao kuweza kuwasaidia mitaji ya kuviendeleza vikundi vyao ili viwaletee tija na kujikwamua na maisha .

    Wakitoa maombi yao kwa Viongozi wa Jimbo hilo huko Mitakawani , wamesema vikundi vingi vinashindwa kupiga hatua kutokana na kukosa mitaji ya kutosha , hivyo wamewaomba kuwaunga mkono ili waweza kufanya shughuli zao kwa ufanisi .

     Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira na mbunge wa Jimbo la Uzini Mhe. Khamis Hamza Chilo , amesma  dhamira ya serikali ni kuviwezesha kiuchumu vikundi vya wajasiriamali ili kuweza kujitegemea.

     Viongozi wa Jimbo hilo wamewaahidi kuwasaidia Wajasiriamali hao pamoja na kuwapatia mafunzo ili kuondoa tatizo la ukosefu wa mitaji linalowakabili. 

 

 

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.