WADAU WA HABARI WATAKIWA KUZINGATIA MUONGOZO WA KURIPOTI MATUKIO YA UCHAGUZI

MWENYEKITI WA BODI SHIRIKA LA UTANGAZAJI ZANZIBAR

    Wadau wa Vyombo vya Habari  na Waandishi wa Habari wametakiwa kuzingatia maudhui ya Utangazaji na kufuata utaratibu wa miongozo ya kuripoti Habari  wakati wa Kipindi cha Uchaguzi.

    Akifungua Mkutano wa Wadau wa Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Bodi Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Ame Khamis katika Kikao Maalum cha Maelekezo ya Wajibu wa Vyombo vya Habari kuzingatia maudhui na muongozo wakati wa Kuripoti Matukio ya Uchaguzi amesema ni vyema Waandishi Wahabari  kufuata Miongozo kama ilivyoekwa  wanapofanya  Kazi zao.

    Katibu Mtendaji Tume ya Utangazaji Zanzibar Suleiman Abdulla Salim  amesema Tume ya Utangazaji Zanzibar ndio Chombo pekee  kinacho husika na usajili wa Vyombo vya Habari hivyo Chombo chochote ambacho hakina Leseni na kusajiliwa hakitoruhusiwa kurusha   Matukio ya Uchaguzi.

   Wakiwasilisha Mada ya wajibu wa Vyombo vya Habari na Muongozo  wa Kuripoti Habari  wakati wa Uchanguzi  Mrajis Tume ya Utangazaji Zanzibar Mohamed Said  na Afisa Sheria Tume Utangazaji Khadija Mabrouki wamesema  Waandishi wanatakiwa kuandika Habari za ukweli na  sahihi ili  kuepuka kuleta uchochezi au  uvujifu wa amani.

   Mrajisi Idara ya Habari Maelezo Jamila Mahmoud Juma  amesema Waandishi wa Habari wote  wanatakiwa kuwa  na Vitambulisho vya Habari Maelezo ambavyo vitamsaidia kuuchukulia Matukio ya Uchaguzi. 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.