VIONGOZI WA DINI WAMETAKIWA KUHUBIRI AMANI.
Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Shekhe Othman Ame Choum amewataka Viongozi wa Dini kuendelea kuhubiri Amani kwa lengo la kukuza uchumi na kuleta maedneleo Nchini.
Naibu Kadhi huyo ameseyasema hayo huko Gombani katika Kongamano la
Kuukaribisha Mwaka Mpya wa Kiislamu 1446 Hijria ,lililowakutanisha Viongozi na Waumini wa Dini ya Kiislamiu .
Amesema suala la uvunjifu wa Amani silakupewa nafasi kutokana na kuwepo kwa Athari kubwa katika Jamii kiuchumi na Kimaendeleo hivyo ni jukumu la Waislam Kuendelea kutunza amani kwa faida yao na Taifa.