MASHEHA WAMETAKIWA KUJUA HAKI NA WAJIBU WAO KWA WANANCHI
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora Tanzania imeendelea kutoa Mafunzo kwa Masheha wa Wilaya ya Mjini yatakayowasadia katika kuwajengea uwelewa wa kusimamia majukumu ya kazi zao za kuwahudumia Wananchi.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Idrissa Kitwana Mustafa amewataka Masheha hao kusimamia vyema na watekelze Majukumu yao kwa kujua nafasi ya haki za Binadamu na wajibu wao katika mazingira yao ya kazi na Jamii kwa ujumla na kufuata misingi ya haki, Kanuni na Utawala bora katika Jamii.