PBZ YAKABIDHI GAWIO LA BIL.7 KWA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

     Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) imekabidhi gawio la Sh 7 Bilioni kwa mwanahisa wake wa pekee Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) kufuatia faida iliyopata katika kipindi cha mwaka 2023. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamiliki asilimia 100 ya hisa za benki hiyo.

BODI MPYA YA PBZ YAZINDULIWA

    Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Dk. Saada Mkuya Salum amewataka Watendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar (Pbz) kuipa ushirikiano Bodi mpya ili waweze kuyapeleka mbele zaidi mafanikio ya Benki hiyo.

    Akizindua Bodi mpya ya Pbz  Dkt.Saada amesema mafanikio yaliyopatikana ni makubwa ukilinganisha na walipotoka ambapo bado kuna fursa katika Soko hivyo anaamini ushirikiano huo utawawezesha kufika lengo la Serikali.  

MABADILIKO YA KASI YAHITAJIKA PBZ

    Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango, imeitaka Benki ya Watu wa Zanzibar Pbz kubadilika ili kwenda kwa kasi zaidi na kufikia malengo ya Serikali.

    Akijitambulisha kwa Uongozi wa Benki ya Pbz Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Juma Makungu Juma amesema pamoja na mafanikio mbalimbali yaliyopatikana na Benki hiyo bado ipo nyuma katika utoaji wa huduma ukilinganisha na Benki nyengine zilizoanzishwa hivi karibuni ambazo zinaonekana kuwa juu.

Subscribe to #Pbz
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.