TAASISI ZA URITHI NA MAMBO YA KALE ZIMETAKIWA KUSIMAMIA MAPATO

Waziri wa Utalii na mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga ameziagiza Mamlaka husika zinazosimamia Urithi na mambo ya kale Zanzibar kuhakikisha wanasimamia mapato ya Serikali kupitia Sekta hizo.

Waziri Soraga akizungumza kwa wakati tofauti katika ziara ya kukaguwa Sekta hizo amesema maeneo hayo yana umuhimu mkubwa katika kuchangia pato la Taifa hivyo amewataka Wakurugenzi Dhamana kuhakikisha wanakaa na Wawekezaji ili kutimiza wajibu wao katika kuchangia pato la Taifa kama walivyo kubaliana katika Mikataba yao.

SMZ KUSHIRIKIANA NA WADAU WA UTALII KUKUZA SEKTA YA UTALII

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kushirikiana na Wadau wa Utalii ili kukuza Sekta ya Utalii Zanzibar.

Akizungumza katika Kikao cha Wadau wa Utalii Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe Mudrik Ramadhan Soraga amesema hatua hiyo itasaidia kukuza Uchumi wa Nchi na kuleta Maendeleo kupitia Sekta hiyo na kuona Utalii unainufaisha Zanzibar katika Nyanja mbali mbali. 

Waziri Soraga amesema atahakikisha Wanashirikiana na ZRA kuimarisha mifumo ya malipo kwa Kielektroniki yanafanyika ili kuongeza Pato la Serikali.

Subscribe to MHE. MUDRIK RAMADHAN SORAGA
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.