SMT KUPATA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI 2 KWA BIASHARA YA KABONI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kupata wastani wa Shilingi Trilioni 2 nukta 4 kutokana na Biashara ya Kaboni ambazo zitachangia kuimarisha pato la Taifa.

Dkt. Jafo ameliarifu Bunge wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru Felix aliyetaka kujua biashara ya Kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani kwenye pato la Taifa tangu iingie Nchini.

SMT KUFANYA TATHIMI YA MAENEO KUKABILIANA NA ATHARI ZA KIMAZINGIRA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Wizara za Kisekta imeanza kufanya tathmini Nchi nzima kubainisha maeneo yanayohitaji kufanyiwa maboresho kukabiliana na athari za Kimazingira.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambwe Mhe. Khalifa Mohammed Issa aliyetaka kujua lini Serikali itafanya utafiti kuyabaini maeneo yaliyoathiriwa na mabadiliko ya Tabianchi.

Subscribe to DKT SELEMANI JAFO
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.