DKT.MWINYI AWATAKA WANASIASA KUSHINDANA KATIKA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka wanasiasa kushindana kuwaletea wananchi huduma bora za kijamii kimaendeleo.

    Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kama yeye amejenga hospitali kila Wilaya na kuboresha huduma mbalimbali za kijamii iwe ni mashindano na siyo kuleta hoja za uvunjifu wa amani.

     Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo wakati wa makabadhiano na ufunguzi nyumba za Wafanyakazi wa Hospitali ya Abdullah Mzee , Mkoa wa Kusini Pemba .

SMZ IMETENGA ENEO LA BANDARI JUMUISHI KUHAKIKISHA USALAMA WA UPOKEAJI NA UGAVI BIDHAA
DKT.MWINYI AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI KUJA KUWEKEZA NCHINI

      Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema  Zanzibar ina miradi mingi inayohitaji Wawekezaji kuja kuwekeza.

     Katika mazungumzo na uongozi wa Kampuni ya Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara na Reli  CCECC kutoka China amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ipo tayari kushirikiana na Kampuni hiyo kutimiza ndoto ya kuijenga upya Zanzibar. 

RAIS DKT.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KAMPUNI YA WAPCOS LIMETED YA INDIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na RK Agrawal Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya ushauri WAPCOS Ltd kutoka Serikali ya India na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 07 Mei 2024.

Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar inahitaji miradi mingi ya uwekezaji katika sekta ya maji na umeme.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi ameishukuru Serikali ya India kwa kuisaidia Zanzibar katika miradi ya maji.

Naye Mkurugenzi RK Agrawal amesema wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika miradi hiyo.

DKT.MWINYI AWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUDUMISHA AMANI NA UTULIVU KWA MAENDELEO YA NCHI

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba wananchi kuendelea kushikamana, kuwa wamoja, kudumisha amani na utulivu ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii nchini.

      Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Dua ya kumuombea Mwanachuoni mkubwa Zanzibar Alhabyb Ahmad Bin Abuubakar Bin Sumeit iliyofanyika Msikiti wa Ijumaa Malindi , Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 22 Aprili 2024.

DKT.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA RAIS WA COMORO

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi kutoka kwa Rais wa visiwa vya Comoro, Azali Assoumani.

    Viongozi hao walikutana leo tarehe 21 Aprili Bweleo, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi .

     Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe 29 Februari, 2024 Dar es Salaam na kuzikwa tarehe 02 Machi 2024 kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja.

SERIKALI KUKABILIANA NA HALI YA UGUMU WA MAISHA KWA WANANCHI

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itachukua jitihada za kukabiliana na hali ya ugumu wa maisha kwa kadri ya hali itakavyoruhusu ili kuwapunguzia mzigo Wananchi.

   Akizungumza na Wazee wa Chama cha Mapinduzi katika Ikulu ya Pagali, amesma kupanda kwa gharama za maisha kunachangiwa na matatizo katika uchumi wa Dunia zikiwemo, vita, kupanda bei kwa bidhaa za nje na baadhi ya Mataifa Duniani kuzuia kuuza bidhaa zao kwa Mataifa mengine.

DKT.MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA KWA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM

    Makamu Mwenyekiti wa CCM  Zanzibar, na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi Amepokea salamu za pole kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa wa Zanzibar wakiongozwa na              Ndg. Mohamed Aboud Mohamed waliofika Ikulu Mnazi Mmoja.

    Wajumbe hao wa Kamati Kuu ya CCM Zanzibar wamesema Msiba huu ni wa wote kwani Marehemu alikuwa amewafundisha wengi mazuri kwa Taifa.   

POLE HAZIJAMALIZA KUMIMINIKA KWA DKT.MWINYI

    Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepokea Salamu za Pole kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara  Abdulrahman Omar Kinana.

    Kinana ametoa Pole hiyo Ikulu Zanzibar, amemueleza Rais Dkt. Mwinyi kuwa Mmsiba  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu wa Awamu ya Pili umewagusa Watu Ndani na Nje ya Tanzania.

DKT.MWINYI AENDELEA KUPOKEA MKONO WA POLE

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameendelea kupokea salamu za pole kutoka kwa Viongozi Wastaafu, Serikali, Ndugu na Jamaa. 

     Hatua hiyo inafuatia Kifo cha Baba ake na Rais Mstaafu Marhum Hayati Ali Hassan Mwinyi.

Subscribe to #Dkt.Mwinyi
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.