SUALA LA UTAFUTAJI WA MAFUTA NA GESI LINAHITAJI MUDA
Mamlaka ya utafutaji na uchimabaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar imesema suala la utafutaji wa rasilima hizo unahitaji utafiti wa kina ili kukamilika kwake na kupata matokeo sahihi kwa zoezi hilo.
Wakitoa uwelewa kwa Watendaji wa Shirika la Mawasiliano Zanzibar kuhusu hatua iliyofikia Mkurugenzi idara ya data Ndg.Mohamed Salum na Meneja wa mamlaka hiyo Ndg. Khamis Juma wamesema hadi sasa kumetangazwa uwepo wa vitalu na maandalizi yake ni kuvitangaza kwa ajili ya wawekezaji kuekeza.